Loading...
title : WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA
link : WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA
WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA
Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
WANAFUNZI watatu wa shule za Sekondari katika Manispaa ya Morogoro wamefariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa miongoni mwao watu wazima baada ya basi dogo aina ya Coaster kugonga treni ya abiria iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha tukio hilo mapema leo kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi karibu na eneo la Ofisi za Mkoa za Tanesco ambapo kipo kizuizi cha kivuko cha treni inapokatisha barabara ya kutoka mjini kwenda Msamvu , Manispaa ya Morogoro.
Alisema dereva aliyekuwa anaendesha basi hilo lenye namba za usajili T438 ABR alikatiza kwenye barabara bila kuchukua tahadhari katika kivuko cha Treni wakati ikiwa inapita kitokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo alisema basi hilo ndogo linalofanya safari zake kati ya Mjini na Kihonda iligonga treni hiyo ya abiria.
Kamanda Matei alisema kuwa katika ajali hiyo wanafunzi watatu, wawili wa wakiume na mmoja wa kike walipoteza maisha na kwamba walikuwa wanasoma Shule za sekondari Tushikamane na Mji mpya.
Kufuatia ajali hiyo alisema polisi inamshikilia dereva wa basi hilo ndogo, Charles Damian Petro (39) mkazi wa Kihonda kutokana na kusababisha ajali iliyopoteza maisha ya wanafunzi hao na kujeruhi wengine kadhaa baada ya kukatiza kwenye kizuizi cha treni bila kuwa na tahadhari.
Kamanda Matei aliwataka wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wakati wanapokuwa wakivuka njia za reli ili kuepusha ajali ambazo mara kadhaa zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva kwa kuzigonga treni.
Naye Mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Frank Jacob alisema , kuwa walipokea walipokea majeruhi 33 na kati yao watatu walifariki dunia wakipatiwa matibabu ambao ni wanafunzi , mmo akiwa ni wa kike na wawili wakiume. Alisema majeruhi 30 wamelazwa katika hospitali hiyo kati yao wanaume ni 10 na wanawake ni 23 na hali zao zinaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa mganga mkuu mkoa huyo kuwa baadhi ya majina ya majeruhi waliolazwa katika wodi namba tatu ya wanawake ni Asha Masud, Rehma Mashaka, Fatuma Aman , Zena Shabani, Salma Said na Asha Omari.
Wengine ni Azama Rajab , Umi Mohamed , Magdalena Mgina , Ratifa Hassani, Florah Clemence, Eveline Mtelani, Asia Omary, Sada Seif . Lucy Lyamba, Nuru Shaban , Eliopa Paulo, Rehema Azizi na Monica Julias.
Mbali na wodi ya wanawake majehuri wengine wanaume walilazwa katika wodi namba mbili akiwemo Yasin Khalid Mkinngiye wanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Tushikamane.
Naye Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo ambaye alifika eneo la tukio hilo alisema, mashuhuda anaeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva huyo.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya kuwa, askari wa reli alizuia magari kwa kunyosha alama ya kibendera chekundu kusimamisha magari lakini dereva huyo aliamua kuyapita yaliyosimama mbele na kufika kizuizi hicho na kabla ya kuvuka akigonga treni hiyo.
Gari hilo liliburuzwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka eneo la tukio na kuangukia pembezoni na kusababisha majeruhi na vifo hivyo.
Alisema treni hiyo ya abiria haikuwa katika mwendo mkali kitendo ambacho kimepunguza madhara mengi licha ya kupoteza wanafunzi watatu.
Umati mkubwa ulijitokeza eneo la ajali ambao pia walienda kuwangalia majeruhi wa ajali hiyo katika Hospitali hiyo ili kuwatanmbua watoto ama ndugu zao wakiwemo walimu wa shule za Sekondari na Msingi.
Basi dogo Daladala lenye namba za usajili T 438 ABR lililokuwa limeigonga treni ya abiria likipelekwa kituo cha polisi
Mamia ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakwa eneo la karibu na Ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro wakiangalia basi dogo Daladala lenye namba za usajili T 438 ABR likiwa limeganga treni ya abiria yenye kichwa namba 88U08 iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu, daladala hiyo ilikuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda ndani yake ikiwa na idadi kubwa wanafunzi wa msingi na sekondari na wananchi.
Basi dogo Daladala lenye namba za usajili T 438 ABR lililokuwa limeigonga treni ya abiria yenye kichwa namba 88U08 iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu, iliyokuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda ndani yake ikiwa na idadi kubwa wanafunzi wa msingi , sekondari na wananchi ikiwa juu ya gari la kubeba vitu vizito la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupelekwa Kituo cha Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.
Basi dogo Daladala lenye namba za usajili T 438 ABR lililokuwa limeigonga treni ya abiria yenye kichwa namba 88U08 iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu.
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii
Hivyo makala WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA
yaani makala yote WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/wanafunzi-watatu-wafariki-dunia-baada.html
0 Response to "WANAFUNZI WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA BASI DOGO KUGONGA TRENI YA ABIRIA MOROGORO, 30 WAJERUHIWA"
Post a Comment