Loading...
title : WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI
link : WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI
WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Ametoa onyo hilo leo mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo.
"Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili."
"Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa CUF Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya Agosti 11. 2017, Waziri Mkuu yupo wilayani Kaliua kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mwamnange kilichopo Wilaya ya Kaliua leo Agosti 11, 2017 .Wananchi hao walisimamisha msafara wake ili kumuomba serekali iwasaidie kupata umeme.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihotubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Veta Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora leo August 11, 2017, ambapo amewataka wananchi waliopewa uraia kuheshimu sheria za nchi vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI
yaani makala yote WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/waziri-mkuu-majaliwa-wananchi-waliopewa.html
0 Response to "WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI"
Post a Comment