Loading...
title : ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO.
link : ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO.
ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Na Mwandishi wetu, Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.
Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.
Hivyo makala ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO.
yaani makala yote ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/zambi-apigia-debe-uwezeshaji-wa-kilimo.html
0 Response to "ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO."
Post a Comment