Loading...

Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

Loading...
Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga
link : Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

soma pia


Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga





Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.


Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.


Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .


‘’ Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa hapa ni takribani 10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta mabadiliko makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.


Pia ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto mwenye vimelea vya bakteria.


Akiwasilisha mada kuhusu muongozo huo , Daktari wa watoto , Jullieth Cosmas ametaja sababu zinazochangia watoto wachanga kulazwa Hospitalini kuwa ni mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) mtoto kushindwa kupumua vizuri pindi anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia wakapi alipozaliwa na mtoto kuumia wakati akizaliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.

Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.

Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.

Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru (kaunda suti) akiwa kwenye mkutano huo leo.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya MNH na wadau mbalimbali.


Hivyo makala Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

yaani makala yote Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/afya-muhimbili-yazindua-mwongozo-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Afya :Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga"

Post a Comment

Loading...