Loading...
title : CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi
link : CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi
CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, kimezifuta barua walizoandikiwa madiwani sita wa Halmashauri ya Moshi, wakitakiwa kujieleza kwa usaliti.
Mbali na kufuta barua hizo zilizokuwa zimeandikwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Moshi, Emmanuel Mlaki chama hicho kimemsimamisha uongozi katibu huyo.
Madiwani hao akiwamo Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila walitakiwa kujieleza kwa madai ya usaliti kwa kumchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri kutoka NCCR-Mageuzi.
Chadema na NCCR-Mageuzi ni vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unajumuisha pia CUF na NLD.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema imesema barua zilizoandikwa na Mlaki ni batili na ameagiza ziondolewe katika rekodi za chama hicho.
“Tunautangazia pia umma kuwa Emmanuel Mlaki amesimamishwa uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake na tunautaka umma kusitisha mawasiliano rasmi ya chama kupitia kwake.”
Hivyo makala CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi
yaani makala yote CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/chadema-yamtimua-katibu-wake-moshi.html
0 Response to "CHADEMA Yamtimua Katibu wake Moshi"
Post a Comment