Loading...

DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA

Loading...
DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA
link : DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA

soma pia


DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA

Na Kajunason/MMG-Handeni-Tanga. 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe amekabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha Kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. 

Akizungumza wakati akikabidhi ardhi hiyo katika kijiji cha Kitumbi, Handeni mkoani Tanga, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo na maendeleo katika kijiji hicho ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli kuendeleza nchi ya viwanda na biashara. Wadau wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza wakiwemo wasanii wa filamu, muziki na wachezaji mpira wa zamani wameamua kushiriki katika maendeleo ya taifa kwa kujihusisha na kilimo tofauti na kazi zao za kila siku za sanaa. 

 "Handeni ni sehemu ambayo korosho, alizeti, ndizi vinakuwa sana na niwaambie tu mapema mwakani kiwanda kutengeneza juisi ya nanasi kinafunguliwa Kwa Msisi, tena kitakuwa na uwezo wa kuchukua tani 80,000 za nanasi kwa mwaka na kitakuwa cha pili Afrika kwa kuzalisha juisi ya nanasi, hapo kazi kwenu kuchangamkia fursa," Alisema Mhe. Gondwe. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, msanii Steve Nyerere alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Gondwe na vingozi wa kijiji kwa kuwapa eneo la kuwekeza katika sekta ya kilimo. 

 "Sisi tunawashukuru wote kwa moyo mliotuonyesha, hatuna cha kuwalipa bali tutapambana kwa nguvu zetu ili kutimiza malengo ya eneo mlilotupa, Uzalendo Kwanza Oyeeee!," alisema Msanii Steve Nyerere. Nae diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid amewakaribisha wasanii hao kwa mikono miwili na kuwaomba wawasaidie kumalizia ujenzi wa zahanati yao ambao umekuwa ukisua sua kutokana na kukosekana kwa fedha.
UZALENDO KWANZA wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe wakielekea katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga, ambapo walipatiwa Mashamba yenye ukubwa wa hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa Kilimo. Picha zote na Kajunason/MMG-Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Godwe akiongea mara baada ya kuwakabidhi ardhi yenye ukubwa wa hekari 282 katika kijiji cha kitumbi kwa wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA. Tukio hilo lilifanyika kijijini Kitumbi, Muheza - Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Msanii Steve Nyerere akitoa shukrani zake za pekee kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kuwakaribisha wana- UZALENDO KWANZA na kuwapatia hekari 282 za ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo katika kijiji cha Kitumbi wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.
Diwani wa Kata ya Kitumbi, Charles Abeid akiwakaribisha wasanii na wadau wengine wanaofanya kampeni ya UZALENDO KWANZA.



Hivyo makala DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA

yaani makala yote DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/dc-handeni-gondwin-gondwe-akabidhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC HANDENI, GONDWIN GONDWE AKABIDHI ARDHI YENYE HEKARI 282 KWA UZALENDO KWANZA"

Post a Comment

Loading...