Loading...
title : DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI
link : DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI
DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI
Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Agness Mtei akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ya namna vitambulisho vya Taifa vinavyotengenezwa mara baada ya kuzinduzi zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Na Mathias Canal, Singida.
Zoezi linalotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi la usajili na utambuzi wa watu wanaoishi katika Wilaya ya Ikungi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea limezinduliwa rasmi huku wananchi wakihamasishwa kutoa ushirikiano katika zoezi Hilo.
Zoezi Hilo litatekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza utekelezaji wake utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa wananchi wapatao 45,599, Awamu ya Pili itakuwa Ni Tarafa ya Sepuka yenye Kata Saba na wananchi wakiwa Ni 49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa 54,887 na awamu ya nne itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla ya wananchi wapatao 35,311.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Akizungumza Katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi kwenye uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa zoezi Hilo linalenga kupata taarifa sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo Yote ya serikali na binafsi kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha Huduma na kuinua hali za watu kutoka kipato Cha chini kwenda Cha Kati.
Alisema umuhimu wa zoezi Hilo Ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususani maeneo ya mipakani, Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Mali hususani Biashara, usalama katika miamala ya kibenki pamoja na kuwezesha wananchi kukopeshana kirahisi, Upatikanaji kirahisi wa pembejeo na zana za Kilimo, na Wananchi katika Kaya maskini kutambulika haraka na kupata misaada kupitia TASAF.
Maafisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi wakiwasalimu wakazi wa kijiji na Kata ya Dung'unyiwakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika. Kulia ni Agness Mtei, Doris Niyukuri na Mary Maputa.
Umuhimu mwingine Ni Upatikanaji wa mikopo ya elimu ya just, Kupunguza ukiritimba katika upatikanaji wa Huduma za Jamii na Kupunguza serikali gharama za kusafirisha daftari la wapinga kura na kuwa na daftari lenye taarifa sahihi za watu na mahali walipo.
BOFYA HAPA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA HABARI NA PICHA ZAIDI
Hivyo makala DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI
yaani makala yote DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/dc-mtaturu-azindua-zoezi-la-usajili-na.html
0 Response to "DC MTATURU AZINDUA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WANANCHI WILAYA YA IKUNGI"
Post a Comment