Loading...

DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN

Loading...
DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN
link : DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN

soma pia


DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN


BALOZI wa Tanzania nchini Marekani Asha-Rose Migiro ni miongoni mwa wajumbe 18, walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, watakaounda Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Upatanishi ya Umoja wa Mataifa. 

Bodi hiyo, iliundwa hivi karibuni baada ya Guterres kusikitishwa na matukio ya mauaji ya raia kutokana na migogoro na vita inayoendelea katika nchi mbalimbali duniani. Kutokana na hali hiyo, aliamua kuanzisha bodi hiyo ya kidiplomasia kwa ajili ya kufanya kazi ya kurejesha amani kupitia upatanisho kwenye nchi zenye migogoro. 

Bodi hiyo imejumuisha vigogo mbalimbali wanaotambulika kimataifa wenye uzoefu wa masuala ya upatanishi na diplomasia na imezingatia jinsia. Kazi kubwa ya bodi hiyo ni kumshauri Katibu Mkuu wa UN juu ya changamoto za upatanishi na kufanya jitihada mbalimbali za upatanishi katika nchi zenye migogoro.

Pamoja na Migiro, wajumbe wengine walioteuliwa kuwemo katika bodi hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel, Rais Mstaafu Olusegun Obasanjo, aliyekuwa Rais wa Chile Michelle Bachelet na Mjumbe wa Baraza la Katiba Sri Lanka Radhika Coomaraswamy. 

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya Usalama, Wanawake na Amani katika chuo kikuu cha Columbia Leymah Gbowee, Mjumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Maafa Raden Mohammad Marty Natalegawa, Mjumbe wa Klabu ya Madrid Roza Otunbayeva na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Knowledge and Freedom (FOKAL) Michele Pierre-Louis. 

Pamoja na wajumbe hao, wengine ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya maafa Jean-Marie Guehenno, Mjumbe wa Baraza la Wanawake viongozi Duniani Tarja Halonen, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Majadiliano ya Haki za Binadamu David Harland na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Asia Noeleen Heyzer. 

Wajumbe wengine ni Mjumbe wa Baraza la Seneti ya Jordan Nasser Judeh, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje nchini Algeria Ramtane Lamamra, Rais Mstaafu wa Timor-Leste Jose Manuel Ramos-Horta, aliyekuwa Mwenyekiti wa watalaamu washauri wa UN kuhusu kujenga amani Gert Rosenthal na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby. 



Hivyo makala DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN

yaani makala yote DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/dr-migiro-arudishwa-tena-un.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DR. MIGIRO ARUDISHWA TENA UN"

Post a Comment

Loading...