Loading...
title : HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA
link : HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA
HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA
HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa vijijini.
Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza, Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na Ngano.
Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto zinazowakabili.
"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana na asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza jana ilkiwa ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto ni Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli .
Hivyo makala HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA
yaani makala yote HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/hospitali-ya-teule-muheza-yapatiwa.html
0 Response to "HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA"
Post a Comment