Loading...
title : JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM
link : JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM
JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen milioni 69 sawa na Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Septemba 1, 2017, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa niaba ya Serikali, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Satoru Matsuyama.
Tukio hilo limekwenda sambamba na kuingia makubaliano kuhusu muda wa kukamilisha mradi huo pamoja na kupeana taarifa ya namna mradi huo utakavyotekelezwa.
Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).
Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Dkt. Mpango amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto), wakisaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida akibadilishana hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakibadilishana hati ya Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini humo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakipeana mkono baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM
yaani makala yote JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/japan-yaipatia-tanzania-msaada-wa.html
0 Response to "JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA AJILI YA KUFANYA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCO, DAR ES SALAAM"
Post a Comment