Loading...

JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Loading...
JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA
link : JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

soma pia


JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Na.Thobias Robert- MAELEZO.

Serikali imelipongeza Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa ushirikiano wake na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za Kilimo Afya na Maendeleo ya Jamii kwa kutumia wataalam na uzoefu kutoka Japan.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Msaidizi wa ushirikiano wa kiufundi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Msafiri Marwa alipokuwa akiwaaga vijana wa kijapani waliokuwa wanajitolea katika sekta ya Kilimo na Maendeleo ya jamii hapa nchini.

“Serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile kuwajengea uwezo Watanzania kupitia ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini Japan na kuleta watu wa kujitolea katika miradi ya maendeleo hapa nchini,” alieleza Bw. Marwa.

Aidha, Bw.Marwa ambaye alimuwakilisha Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bi. Suzani Mlawi aliipongeza Japan kwa kutumia rasilimali watu pamoja na rasilimali fedha kupitia JICA kufadhili utoaji wa huduma za kijamii jambo ambalo ni kipimo cha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Amewapongeza vijana wa kijapan kwa kazi nzuri waliyoifanya hapa nchini katika kipindi chote cha miaka miwili ya kuwahudumia watanzania hasa katika sekta ya Kilimo na Afya.

“Kwa niaba ya serikali niwapongeze vijana wote mliokuja hapa nchini kwa kufanya kazi na jamii ya Watanzania, mmefanya kazi kwa jitihada kubwa wakati mwingine katika mazingira magumu, niwahakikishie kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha mazingira ya ushirikiano ili kuendeleza uhusiano ” alifafanua Marwa.
Mkurugenzi Msaidi wa Ushiririkiano wa Kiufundi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Msafiri Marwa akimkabidhi zawadi kijana wa Kijapan aliyemaliza muda wake wa kujitolea hapa nchini Bw. Yusuke Sakakibara.
Mkurugenzi Msaidi wa Ushiririkiano wa Kiufundi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Msafiri Marwa akimkabidhi zawadi kijana wa Kijapan aliyemaliza muda wake wa kujitolea hapa nchini Kyoko Tada katika hafla ya kuwaaga vijana watatu wa kijapan waliomaliza muda wao wa kujitolea hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Raia wa Japan waliokuwa wakijitolea nchini kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wakiwa katika hafla ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Yusuke Sakakibara akiifanya Wilayani Masasi, Shu Sato, Kyoko Tada Mratibu wa vijana wa kujitolea Kutoka JICA nchinI Tanzania Bw. Ichiro Owa mara baada ya hafla kuwaga leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Paschal Dotto – MAELEZO



Hivyo makala JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

yaani makala yote JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/jica-yapongezwa-kwa-kudumisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA"

Post a Comment

Loading...