Loading...
title : M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE
link : M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE
M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Wanafunzi wa shule ya Sekondali Sandula iliyopo wilayani Mbozi imeepukana na changamoto za ukosefu wa umeme pindi wanapojisomea nyakati za usiku kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya umeme wa Jua 'Solar' kutoka kampuni ya M-Kopa ikiwa ni mara ya pili kutoa msaada huo katika shule ya sekondari hiyo.
Msaada huo umefanyika katika Shule ya Sekondari Sandula Wilayani Mbozi kwa mara ya pili na shule zingine zilizonufaika na msaada huo ni shule ya sekondari Mwinyi iliyopo Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni kwa ajili kuongeza ufaulu katika shule hizo kwa kujisomea zaidi katika nyakati za usiku na kuondokana na matumizi ya vibatari vya mafuta ya Taa.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya Umeme wa Jua , Meneja Mauzo M-kopa Richard Machera amesema kuwa kwa Shule ya Sandula uligharimu zaidi ya sh. milioni 4.9 kwa kununua taa za LED sola 36, Chajazasimu, Betri za kuhifadhi nguvu ya Jua Tisa (9), Paneli Tisa (9), Tochi Tisa (9) na redio za kisasa za sola Tisa (9).
Vifaa hivyo vimefungwa kwenye madarasa mawili, Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Mwalimu Mkuu Msaidizi pamoja na Mabweni.
Vifaa hivyo vimefungwa kwenye madarasa mawili, Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Mwalimu Mkuu Msaidizi pamoja na Mabweni.
Mwalimu Mkuu washule ya sekondari Sandula, Witson Mtafya amesema msaada huo utasaidia wanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea na kufanya mijadala kwenye vikundi kwa fasihi zaidi na hatimaye ufaulu wao utaongezeka.
Meneja Mauzo M-kopa, Richard Machera akikabidhi Msaada huo vifaa vya umeme wa jua kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Sandula Witson Mtafya katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sandula wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .
Walimu wa shule wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mauzo M-Kopa, Richard pamoja na wageni waalikwa wengine katika picha ya pamoja. pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .
Hivyo makala M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE
yaani makala yote M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/m-kopa-yaipiga-jeki-shule-ya-sekondari.html
0 Response to "M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE"
Post a Comment