Loading...

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

Loading...
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA
link : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

soma pia


MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

Mwambawahabari

7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi mkutano wa  Majaji  na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
5
Majaji  na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa  Majaji  na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA). Makamu wa Rais alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”.
Kwa miaka mingi mmeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola, alisema Makamu wa Rais.
Aidha, mkutano huo uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli. “Naamini kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza Makamu wa Rais.
Pia Makamu wa Rais alisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sheria.  Aliwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.
Mwisho Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa  kuhakikisha inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa.  
Imetolewa na :-
Ofisi ya Makamu wa Rais


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa-siku.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SIKU 5 WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA"

Post a Comment

Loading...