Loading...
title : Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro
link : Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro
Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro
Baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo.
Wadau wakifuatilia hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath, akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Regina Chonjo, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini wa makubaliano ya Uwekezaji katika Machinjio ya Kisasa ya Nguru mkoani Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
Eneo litakalotumika kupitishia ng'ombe wakati wakienda katika machinjio hayo.
NA MWANDISHI WETU, Mvomero-Morogoro
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa Dola za kimarekani Milioni 3.90 katika kiwanda cha machinjio na usindikaji nyama cha Nguru ‘Nguru Hills Ranch Limited’ kilichoko nje kidogo ya Morogoro Wilaya ya Mvomero.
Akizunguza katika uwekaji wa saini kwenye mkataba wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, alisema uwekaji wa saini umefikiwa baada ya tathini ya kina iliyofanywa na mfuko huo.Alisema mfuko umejiridhisha kuhusu usalama wa rasilimali za wanachama kwenye uwekezaji huo.
“Tunatambua kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda lakini LAPF imeona fursa hii ni moja wapo ambayo inakidhi vigezo vyote vya ajenda ya uwekezaji”alisema Sanga.
Alisema LAPF imewekeza kwenye kiwanda hicho kwa ubia na kampuni ya ‘Eclipse Investments LLC’ inayotokana na kampuni tanzu ya Zubair Corporation ya Oman na kampuni ya ‘Busara Investments LLP’ na kufanya wabia kuwa watatu.
“Kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na LAPF ni USD 3.9 Milion ambayo ni sawa na asilimia 39 ya hisa za kampuni,ambapo Eclipse Investments LLC inaa hisa asilimia 46 na Busara Investments LLP ina hisa asilimia 15”alisema Sanga.
Alisema kiwanda hicho kina ukubwa wa ekari 6,000 ambapo ekari 1,200 zimejengwa miundombinu ya malisho ya mifugo kwa kipindi kisichopungua siku 90 kwaajili ya kuwanenepesha na kuwapa ubora kabla ya kuchinjwa.
Sanga alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo kuchinja na kuchakata ng’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kusafirishwa mara moja.
“Nyama itakayozalishwa kwa kiwango kikubwa itasafirishwa nje kwenye nchi za mashariki ya kati na mashariki ya mbali ambako soko ni kubwa na Oman”alisema Sanga.
Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 500 na nyingine zisizo za moja kwa moja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vingine.
Hivyo makala Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro
yaani makala yote Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/matukio-lapf-watia-saini-mkataba-wa.html
0 Response to "Matukio : LAPF Watia saini Mkataba wa Uwekezaji katika kiwanda cha Machinjio na Usindikaji Nyama cha Nguru ,Morogoro"
Post a Comment