Loading...
title : MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI
link : MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI
MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI
.....'I am a God fearing person who believes in, and endeavours to do, justice to all irrespective of their status in society.....'
Mzaliwa wa Januari 12, 1951, Jaji wa Mahakama ya juu nchini Kenya, David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti na kuamuru kurudiwa ndani ya siku 60 zijazo. (Land Mark Case).
Wakenya na wadau wengine kwingineko duniani wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara huru ya mahakama.
Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day Adventist Church (SDA).
Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa waumini wa kanisa hilo.
Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya siku ya Sabato kuisha........kama mna kumbukumbu hii pia iliwahi kutokea kwa Waziri mkuu wa zamani wa Israel Bwana Ariel Sharon ambaye aliondoka mkutanoni majira ya saa kumi na mbili baada ya sabato kuingia kuhu akimwacha Clinton kutoamini macho yake (Wayahudi na sabato huwaelezi kitu).........
Wafaransa pia hawatamsahau Benjamin Netanyahau kwani baada ya kuandaa itifaki zote za kumpokea walijikuta wakiambiwa kwamba hangeweza kwenda nchini humo Ijumaa jioni HADI SABATO ITAKAPOKWISHA ...........yaaani kesho yake jumamosi tena baada ya jua kuzama.
Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo lakini yeye aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake. Jaji Maraga alifuzu kama wakili miaka 40 iliyopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kujitegemea.
Hivyo makala MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI
yaani makala yote MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mfahamu-japo-kwa-uchache-jaji-david.html
0 Response to "MFAHAMU JAPO KWA UCHACHE JAJI DAVID MARAGA -MSABATO MWENYE IMANI KALI"
Post a Comment