Loading...

Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China

Loading...
Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China
link : Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China

soma pia


Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China

Mamia ya wadau wa sanaa wamejitokeza kwa wingi Jumanne hii jioni katika Uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kumuaga msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto ambaye ameelekea nchini China kwaajili  ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la utalii wa sanaa duniani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Kitendawili alitangaza katika mitandao yake ya kijamii kwamba atasafiri Jumanne hii kuelekea nchini China hali iliyopelekea mashabiki wengi kumimika uwanjani hapo kwaajili ya kumuaga.

Akiongea na waandishi waliojitokeza uwanjani hapo, Mpoto alisema anawashukuru mamia ya watu waliojitokeza uwanjani hapo kwaajili ya kumuaga kwenda kuiwakilisha nchi katika masuala ya kiutalii nchini China.

“Sikutegemea kama watu watakuwa wengi hivi, huu ni upendo wa dhati sana na nawashukuru sana kwa moyo huo na upendo mliouonyesha, nakwenda China kwaajili ya Watanzania, sio Mpoto lakini nakwenda kuuonyesha ulimwengu kwamba Tanzania tuna utajiri wa sanaa, Tanzania tuna makabila zaidi ya mia moja na ishirini hiki ni kitu kikubwa sana, tunaenda kuwatambia usalama tuliokuwa nao,” alisema Mrisho.

Muimbaji huyo amedai haikuwa kazi rahisi kupata kazi hiyo na kuwa muakilishi pekee wa Tanzania kwenye maadhimisho hayo ya utalii duniani ambayo yanawakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

Aliongeza, “Mungu bado anaendelea kutuona, kati ya nchi zote za Afrika ni nchi tatu tu ambazo zimepata mualiko huu ikiwemo Tanzania na Kenya. Hii ni ishara nzuri sana duniani na Afrika nzima kwa sababu wadau ambao watatembelea mahadhisho hayo washuhudia vitu vyetu vya asili, ngoma, nyimbo, ala za muziki pamoja na mitindo mbalimbali ya upigaji wa ngoma,”

Alisema safari hiyo imewezeshwa na  Ubalozi wa Tanzania China, Wizara ya Utamaduni, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA, TTB, BASATA pamoja na Leopard Tours.


Hivyo makala Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China

yaani makala yote Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mrisho-mpoto-kuiwakilisha-tanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mrisho Mpoto kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duniani nchini China"

Post a Comment

Loading...