Loading...
title : MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI
link : MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI
MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI
Na Agness Francis Blogu ya jamii.
Katika tamasha la tamasha la muziki Mnene lililokonga nyoyo za mashabiki ambalo limefanyika katika ukumbi wa New Msasani Jijini Dar es Salaam ambapo wasanii kama Chidi Benzi, Nuhu Mziwanda, Izzo Business, Bob Junior, Makomando pamoja na Kayumba Asosiye mshindi wa BSS walitoa burudani ya kutosha kwa wakazi hao wa Kinondoni.
Hata hivyo Michuzi Blog imezungumza na msanii Kayumba Asosiyee ambaye mpaka hivi sasa yupo chini ya meneja wake Mkubwa Fella ametanabaisha kuwa kuwepo kwa tamasha hilo la Mziki nene linasaidia kukuza vipaji vya wasanii chipukizi vilivyolala.
Vile vile msanii huyo amesema kuwa changamoto ya muziki wa sasa mchuano umekuwa mkali sana kwa sababu mashabiki wanajua muziki mzuri, inabidi kupambana ili kuhakikisha unatoa kitu chenye ubora, na amewaahidi mashabiki wake wake mkao wa kula anatarajia kutoa ngoma yake hivi karibuni.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Chidi Benzi akiwaburudisha mashabiki wake na kuwa acha midomo wazi Kwa kazi nzuri alioifanya katika tamasha la muziki Mnene katika klabu ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Izzo Business akifanya yake jukwaani kuwaburudisha mashabiki wake na wapenzi wa hip hop waliojitokeza Kwa wingi katika tamasha hilo la muziki mnene katika klabu ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nuhu Mziwanda akizima kiki na kuwasha muziki katika kuhakikisha wakazi wa Kinondoniwanapata Burundi kabambe akiimba nyimbo yake mpya ambayo inajulikana kama bao la ushindi katika tamasha hilo la muziki mnene katika klabu ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa kizazi kipya kundi La Masada sita wakitia burudani Kwa kuimba na kucheza kuwaburudisha wazi wa maeneo hayo ambao hawakuachwa salama Kwa shoo nzuri iliofanywa na wadada hawa katika tamasha la muziki mnene katika klabu ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mashabiki na wakazi wa Kinondoni waliojitokeza Kwa wingi kushuhudia shoo ya kukata na shoka kutoka Kwa wasanii Mbalimbali wa hapa nchini wakitoa burudani kwao katika tamasha la muziki mnene katika klabu ya New Msasani Jijini Dar es Salama. Picha na Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Hivyo makala MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI
yaani makala yote MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mziki-mnene-efm-haujawaacha-salama-kwa_24.html
0 Response to "MZIKI MNENE EFM, HAUJAWAACHA SALAMA KWA WAKAZI WA KINONDONI"
Post a Comment