Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka. - Hallo rafiki
SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts
makala afya,
makala general,
makala kisiasa,
makala kitamaduni,
makala kiuchumi,
makala mambo mapya,
makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.
title :
Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka.link :
Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka.
Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka.
Na Benedict Liwenga-WHUSM
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ufanisi wao wa kazi huku akiwataka kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuleta maendeleo katika soka.
Mhe. Wambura ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za Shirikisho hilo ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ikiwemo changamoto za shirikisho pamoja na maendeleo ya soka nchini.
Akiongea na Viongozi mbalimbali na wadau wa soka katika ziara yake hiyo, amesema kwamba anaridhishwa na kazi wanazofanya TFF na amewapongeza kwa kupata uongozi mpya wa Shirikiho hilo na kuwasisitizia kujenga mahusiano ya karibu na wadau wa soka ikiwemo kuwajengea uwezo vijana ili kukuza vipaji vyao na hatimaye kuleta heshima kwa Taifa.
“TFF hongereni kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya, hakika mnajitahidi sana lakini niwaombeni muzidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kwamba tunapata maendeleo mazuri katika soka, hivyo ni vema mkawa mnajenga mawasiliano na Viongozi wa Serikali mara kwa mara ili na sisi tupate kujua mambo yanayofanyika”, alisema Mhe. Wambura.
Sambamba na hilo, Naibu Waziri Wambura amesisitiza juu ya suala la ugawaji wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea katika maeneo mbalimbali nchini huku akisema kuwa, ugawaji huo uwe wa uwiano sawa ili pasitokee eneo moja likawa linakosa vifaa hivyo kwakuwa vijana wote ni Watanzania na wana haki sawa ya kushiriki katika michezo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Bw. Kidao Wilfred amesema kwamba, TFF imejitahidi kuwasaida vijana mbalimbali wakiwemo Serengeti Boys kwa kuwapatia vitendea kazi na amepokea ushauri wa Naibu Waziri wa kuendelea kujenga uhusiano wa karibu na Serikali ili kukuza soka nchini.
“TFF tumekuwa tukiwaandaa vijana mbalimbali ili kuweza kuwapata wenye vipaji vizuri na tumepanga kuwa vijana hawa waweze kupatiwa shule ambapo watakuwa wanajifunza masuala mazima ya soka na nikieleze tu Mheshimiwakwamba ushauri wako wa kujenga ushirikiano na Serikali tumeupokea na tunaufanyia kazi”, alisema Wilfred.
 |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akiongea na Vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia wakati alipotembelea Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam. |

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura(aliyekaa katikati) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwemo wengine toka Wizarani wakiwaangalia vijana wa Serengeti Boys wanaochipukia katika Viwanja vya Karume 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura(kushoto) akisalimiana na Kocha Kim Paulsen wakati alipotembelea ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 18 Septemba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
Hivyo makala Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka.
yaani makala yote Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/naibu-waziri-anastazia-wambura.html
Related Posts :
MIILI ILIYOPATIKANA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE SASA YAFIKIA 224*Waziri asema uwezo wa kivuko ilikuwa kubeba watu 101 lakini siku ya tukio kilibeba watu 265
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Uje… Read More...
NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA*Serikali yaamua kutoa Sh.500,000 kwa kila mfiwa kusaidia mazishi, Waziri Mkuu aongoza maziko ya pamoja
Na Said Mwishehe,Globu ya jam… Read More...
HUZUNI KUBWA KWA TAIFA,MIILI YA WATU ... RC MONGELA AELEZA NAMNA WANANCHI WALIVYOFANIKIWA KUOKOA WATU 40 WAKIWA HAI* Ni katika tukio la kuzama kivuko cha MV.Nyerere, Mbunge wa Ukerewe aomba kivuko cha uhakika
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa… Read More...
Inna lillah wainna rajun.Dk.Malik Abdallah Juma Amefariki Dunia leo Asubuhi.Innaa lillahi Wa Inna ilayhi rajiuwn. Dr Malik Abdallah Juma ameshafariki asubuhi hii. Maziko yatakua al asir kijijini kwao msonge (namba Sa… Read More...
MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM WAAGWA RASMI
Na Mary Gwera, Mahakama
JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama i… Read More...
0 Response to "Naibu Waziri Anastazia Wambura aipongeza TFF, Aitaka izidi kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo ya Soka."
Post a Comment