Loading...
title : Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa
link : Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa
Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa
Serikali imesisitiza umuhimu wa mafunzo zaidi kwa wataalamu wa ukaguzi na udhibiti ili kuhakikisha dawa zinazoingizwa na kutengenezwa nchini zina ubora kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazozikabili nchi nyingi barani Afrika katika kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya ni ukosefu wa wataalamu wa kutosha wa ukaguzi wa dawa hivyo mafunzo ya wataalamu hao hayana budi kupewa kipaumbele.
“Tanzania tunaagiza asilimia themanini ya mahitaji yetu ya dawa na kutengeneza kiasi kilichobaki hivyo suala la weledi katika ukaguzi na udhibiti wa dawa ni jambo linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa” Dk. Mpoki alisema.
Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tisa ya ulinganishaji wa viwango vya dawa kwa wakaguzi na wataalamu wa udhibiti wa dawa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Bw. Hiiti Sillo akitoa maelezo ya utangulizi kwa washiriki.
Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki akisisitiza jambo katika hotuba yake ya ufunguzi.
Picha ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt. Ulisubisya Mpoki (wa tatu kushoto, msitari wa mbele), akiwa na waratibu, na washiriki wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.
Hivyo makala Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa
yaani makala yote Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/serikali-yasisitiza-umuhimu-wa-mafunzo.html
0 Response to "Serikali Yasisitiza Umuhimu wa Mafunzo Zaidi Kwa Wakaguzi wa Dawa"
Post a Comment