Loading...
title : Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni.
link : Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni.
Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni.
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Kituo cha radio cha Efm kimewatembelea wakati wa Kigamboni pamoja na kufanya vipindi moja kwa moja kupitia radio hiyo na kusikiliza changamoto mbalimbali za wakazi na kuzifanyia utatuzi ukiwa pia lengo ni kuwa karibu na wasikilizaji wao.
Tamasha hilo la muziki Mnene Njendani limehudhuriwa na Mkuu wa wilaya Kigamboni Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi Manispaa ya Kigamboni Stephen Katemba wakiambatana na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ili kuweza kuongea na wananchi moja kwa moja kupitia Kituo cha radio cha Efm katika Viwanja vya Machava Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Viongozi nao wa meweza kuzungumza na wakati wa Manispaa kisikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi nao wa Kigamboni waliojitokeza kwa wingi katika Viwanja hivyo.
Vile vile pia kituo hicho kimelenga hasa kukuza vipaji chipikizi vya miziki maarufu kwa jina la Singeli, kwa kufanya mashindano na kwa atakae ibuka Kidedea kati ya washiriki nao atapata fursa ya kurekodi kazi zake bure kwa gharama za kituo hicho cha redio ya Efm.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa(kushoto) akisalimiana na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita(kulia) katika tamasha hilo la Muziki Mnene njendani lililokuwa linafanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akizungumza na wakazi wa Kigamboni katika kipindi cha Joto la asubuhi ambacho kilirushwa moja kwa moja kutoka Viwanja vya Machavya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Watangazaji wa kipindi cha joto la asubuhi wakiongozwa na Gerard Hando pamoja na Maulid Kitengewakirusha kipindi hicho mubashara kutoka katika Viwanja vya Machava Kigamboni.
Watangazaji wa kipindi cha uhondo wakiongozwa na Dina Marius wakirusha kipindi hicho mubashara kutoka wiwanjani hapo sambamba na kutoa burudani kwa mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi katika Tamasha Njendani Viwanja vya Machava wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mtangazaji wa kipindi cha Sport HQ, Tunnu Shenkome akizungumza na mashabiki wa timu ya Yanga Fc, Simba Fc pamoja na Azam Fc wakionyeshana tambo kila mmoja akijinadi kuwa timu yake ndio itakayoibuka kidedea kunyakua kombe hilo la VPL katika msimu huu.
Msanii wa muziki wa Singeli, Dogo Niga akitoa burudani kabambe kwa wakazi wa Kigamboni katika tamasha la Njendani lililofanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni.
Mashabiki wa Efm watu wazima kwa watoto walijitokeza kwa wingi kupata burudani pamoja na kuonana na Watangazaji mbalimbali wa kipindi vya radio hiyo katika tamasha la Njendani lililofanyika kwenye Viwanja vya Machava Kigamboni. (Picha na Na Agness Francis, Blogu ya Jamii)
Hivyo makala Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni.
yaani makala yote Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/tamasha-la-efm-njendani-lakonga-nyoyo.html
0 Response to "Tamasha la Efm Njendani lakonga nyoyo za mashabiki wao Kigamboni."
Post a Comment