Loading...

TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM

Loading...
TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM
link : TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM

soma pia


TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM


 
Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.

Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.

Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.

Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.

Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.

“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.

Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.



Hivyo makala TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM

yaani makala yote TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/tanesco-yakabidhi-nyumba-mbili-za_7.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM"

Post a Comment

Loading...