Loading...

WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI

Loading...
WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI
link : WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI

soma pia


WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI

Wamiliki wa Showroom za kuuza Magari leo wamepelekwa Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone) kwaajili ya kukagua  eneo hilo na kuonyeshwa namna ya kumilikishwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema eneo hilo litamilikishwa kwa Wamiliki wa Showroom kwa Muda wa Miaka Mitatu ya Mwazo Bure kisha Baada hapo watawekewa utaratibu wa Malipo.

Amesema Wamiliki hao watatakiwa kutoa kiasi cha Shilingi 300,000 kama dhamana ya kuonyesha nia. Amesema kuwa ukubwa wa eneo lilitengwa kwaajili ya Showroom ni Square Meter 750,000 ambapo lipo eneo lingine la ziada lenye ukubwa wa kiasi cha Square Meter zaidi ya 300,000.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya Kigamboni Rahel Mhando amesema mradi huo ni fursa kubwa ya Maendeleo kwa Wilaya hiyo. Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kubuni Mpango huo ambao pia utafanya Wilaya ya Kigamboni kuwa kwenye mpangilio Mzuri.

Nae Salim Chicago ambae ni mmiliki wa Showroom amesema Mpango huo utawapa unafuu wa kupata huduma zote ikiwemo TRA, TPA,BIMA,SUMATRA,Kituo cha Polisi na huduma za Kibank ndani ya eneo moja. Aidha amesema Mpango huo utawarahisishia kupata Wateja wengi na wa uhakika kutoka ndani na Nje ya Nchi.
Hata hivyo amesema utaratibu huo utawawezesha kulipa kodi ya Serikali na kuwabana wale Wafanyabiashara wanaofanya biashara za magari kwenye maeneo bubu.

Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa agizo la kuwataka wenye Showroom na Yard za kuuza Magari kuhakikisha wanahamia Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Showroom kabla ya Mwezi January Mosi mwakani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (wakwanza kushoto) akizungumza na wamiliki wa Showroom za kuuza Magari katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone).
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (katikati) akiwaonesha wamiliki wa showroom eneo lililotengwa kwaajili ya biashara ya magari Kigamboni jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Hivyo makala WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI

yaani makala yote WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/wamiliki-wa-showroom-waonyeshwa-eneo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAMILIKI WA SHOWROOM WAONYESHWA ENEO LILILOTENGWA KWAAJILI YA BIASHARA YA MAGARI KIGAMBONI"

Post a Comment

Loading...