Loading...

Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro

Loading...
Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro
link : Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro

soma pia


Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza hatua ya mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini kuwekeza kwenye sekta ya viwanda huku akitoa wito kwa jamii hususani vijana kuhakikisha wanaonyesha uzalendo kwa kujitolea kwa vitendo kuunga mkono jitihada hizo zinazolenga kutatua tatizo la ajira na kuinua uchumi wa taifa.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro mara tu baada ya kuongoza zoezi la upandaji wa miwa ikiwa ni ishara ya kuunga mkono mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi II unaotekelezwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding unaofanyika katika gereza la Mbigiri, Dakawa mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara alipotembelea shamba la kubwa la miwa linaloandaliwa ikiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi II unaotekelezwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding unaofanyika katika gereza la Mbigiri, Dakawa mkoani Morogoro.

"Pamoja na kutoa pongezi kwa mifuko yetu ya hifadhi ya jamii hapa nchini kwa kuitikia vema wito wa serikali ya awamu ya tano katika uwekezaji wa viwanda vyenye tija kwa taifa, kipekee nitoe wito kwa jamii hususani vijana kuhakikisha wanaunga mkono jitahada hizi kwa kujitolea ujuzi na maarifa katika kufanikisha adhma hii ya serikali inayolenga kuwanasua kutoka kwenye uhaba wa ajira,'' alitoa wito.

Wito huo wa Waziri Mkuu ulikuja kufuatia kuguswa na uzalendo ulioonyeshwa na vijana wasomi sita kutoka mikoa mbalimbali walioamua kuweka kambi kwenye eneo hilo Mbigiri wakilala chini ya miti lengo likiwa ni kuunga mkono jitiahada za ujenzi wa kiwanda hicho kwa kushiriki bila malipo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa kiwanda hicho ikiwemo kubuni mchoro uliotumika katika moja ya jengo litakalotumika kujengwa kiwanda.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio wakati wa ziara hiyo.

"Vijana hawa ambao kwa sasa wamepatiwa maturubai ya kujihifadhi wamekuwa mfano wa kuigwa na wenzao nchi nzima na nitazifikisha salamu zao kwa muheshimiwa Rais ajue jitiahada zake zinatafsiriwa vyema sana na vijana wazalendo wa taifa hili,'' alisisitiza.

Akizungumzia mradi huo Waziri Mkuu alisema pamoja na kumaliza tatizo la uhaba wa sukari hapa nchini, pia utapunguza tatizo la ajira sambamba na kukuza uchumi wa nchi. 

Ili kuhakikisha wananchi wanakuwa kwenye nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kuzalisha malighafi kwa ajili ya kiwanda hicho Waziri Mkuu aliutaka uongozi wa mkoa huo kuhakakikisha wanapita wilaya nzima ya Kilosa unapotekelezwa mradi huo kuhakikisha hakuna mashamba pori zoezi litakaloambatana na unyang'anyaji wa mashamba yasiyoendelezwa kutoka kwa wamiliki wake na kisha kukabidhiwa kwa wananchi wayatumie kwa kilimo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) pamoja na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) wakiongoza zoezi la upandaji wa miwa ikiwa ni ishara ya kuunga mkono mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi II unaotekelezwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding unaofanyika katika gereza la Mbigiri, Dakawa mkoani Morogoro. Kulia, akishirikiana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe.

"Na kwa wale wananchi wanaolima kwenye eneo la magereza utumike utaratibu mzuri waweze kupata mashamba kwenye eneo la magereza waendelee na kilimo hiki cha miwa ili kulisha kiwanda licha ya kuwa umiliki wa ardhi utabaki kuwa ni wa jeshi la magereza,'' alifafanua.

Mradi huo unaolenga kuzalisha tani 50 za sukari kwa mwaka ni sehemu ya mradi mkubwa unaotekelezwa na mifuko hiyo katika eneo la Ngerengere, Wilaya ya Morogoro Vijijini unaofahamika kama Mkulazi I ambao unaolenga kuzalisha tani 200,000 za sukari kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 katika hatua ya awali.



Hivyo makala Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro

yaani makala yote Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/waziri-mkuu-awapongeza-nssf-ppf-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Mkuu awapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri mkoani Morogoro"

Post a Comment

Loading...