Loading...
title : BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN
link : BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN
BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amesema uzoefu wa Sweden wa miaka mingi katika kuendesha serikali za Mitaa unaweza kuisaidia Zanzibar katika kipindi hiki cha ugatuzi.
Balozi Seif amesema hayo afisini kwake vuga wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa watu wanane kutoka sweeden ukiongozwa na Spika wa Manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman ambaye yupo nchini kwa ziara ya wiki moja.
Amesema Zanzibar hivi sasa inapitia katika kipindi cha mageuzi ya serikali za mitaa unaojulikana kwa jina la ugatuzi ili kuyafanikisha mageuzi hayo ni vyema kujifunza kutoka nchi mbali mbali zenye uzoefu.
Balozi Seif amefurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall na kutaka uhusiano huo uimarishwe zaidi. Naye Spika wa manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman amesema Manispaliti yake iko tayari kubadilishana uzoefu na Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu.
Akielezea uhusiano uliopo kati ya Manispaliti yake na Wadi ya Makunduchi, Bi Arianne amesema ameridhishwa na uhusiano huo ambao unaimarika siku hadi siku. Wakati huohuo spika wa baraza la wawakilishi mh zubeir ali maulid amesema ujio wa wa ujumbe huo ni hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano katika masuala muhimu ya maendeleo.
Akielezea shughuli zinazo fanywa ba baraza la wawakilishi mh zubeir amesema ni pamoja na kutunga shera, kupitisha bajeti, masuali na majibu pamoja na kupitisha mipango ya maendeleo. Nae spika wa manispaa ya sundsval ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuahidi kuimarisha uhusiano kwa wawakilishi katika kubadilishana mawazo katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.
Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kusikiza kipindi cha masulaa na majibu katika kiao cha baraza la wawakilishi kichoendelea na kutembelea sehemu mbali mbali za baraza ikiwepo chumba acha hansard.
Hivyo makala BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN
yaani makala yote BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/balozi-seif-ali-iddi-akutana-na-ujumbe.html
0 Response to "BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN"
Post a Comment