Loading...
title : Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora
link : Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora
Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora
Thobias Robert – Maelezo
Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
“Chuo cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo akitoa taarifa ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na menejimenti ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora
yaani makala yote Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/bodi-ya-tpsc-yaagizwa-kusimamia-utoaji.html
0 Response to "Bodi ya TPSC Yaagizwa Kusimamia Utoaji wa Elimu Bora"
Post a Comment