Loading...

DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.

Loading...
DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.
link : DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.

soma pia


DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.

Mwambawahabari


Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  aliyesimama akiongea na  wanafunzi wa Uuguzi na  Ukunga pamoja  na wadau mbalimbali  wa  sekta ya afya  hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi
pix 2
Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  kulia akipata maelekezo kuhusu uuguzi na ukunga kutoka kwa  mfanyakazi wa Chama cha Uuguzi na Ukunga Bw. Stephano Simba kushoto alipotembelea banda lao wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi
pix 3
Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  wa pili  kulia akikata utepe baadhi ya vitabu kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa  Ukunga salama  wakati wa uzinduzi huo  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi  wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda.
pix 4
Mkurugenzi wa  mradi wa Ukunga salama Dkt. Julius Masanika  akiongea na  wanafunzi wa Uuguzi na  Ukunga pamoja  na wadau mbalimbali  wa  sekta ya afya  hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi .
pix 5
Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akisalimiana na Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga  Bukumbi  Bi. Rose Julius ambaye anafadhiliwa na  mradi huo  mahitaji yake ikiwamo pamoja na ada wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi .
pix 6
Mkuu wa  Chuo Cha Uuguzi na ukunga SCIMVE  Bw. Yohana Ngwandu  akiongea na  wanafunzi wa Uuguzi na  Ukunga pamoja  na wadau mbalimbali  wa  sekta ya afya  hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi
pix 7
Wanafunzi wa Uuguzi na  Ukunga pamoja  wakimsikiliza kwa amkini Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi
pix 8
Baadhi ya Wasanii wa Kikundi cha sanaa Cha  wakiigiza mama mjamzito anaelekea kituo cha kutolea huduma ya afya mapema kwa ajili ya kujifungua salama wakati wa uzinduzi wa  mradi wa Ukunga salama  uliofanyika leo  jijini Mwanza katika chuo cha  wauguzi na wakunga Bukumbi.
9
Naibu Waziri  wa Afya, Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akikabidhi matunda kwa baadhi ya wazee alipotembelea kambi ya wazee Bukumbi jijini mwanza.
Picha na WAMJW-MWANZA
………………….
NA WAMJW-MWANZA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa wadau wa sekta ya afya na watoa huduma za afya hasa wauguzi na wakunga wanatakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa na kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives) uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi kilichopo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewaonya wakunga na wauguzi wenye  tabia ya kutumia lugha chafu kwa wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga Salama nchini Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Uuguzi na Ukunga  katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa na mradi huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa Ukunga salama unaojulikana kama “More and Better Midwives”  ambao umeshirikisha  taasisi isiyo ya Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka Chama cha wakungwa  Canada(CMA) na Chama cha wakungwa  Tanzania TAMA pia alitembelea Zahanati ya Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa .


Hivyo makala DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO.

yaani makala yote DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dkt-ndugulile-asisitiza-kuokoa-maisha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DKT. NDUGULILE ASISITIZA KUOKOA MAISHA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO."

Post a Comment

Loading...