Loading...

DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU

Loading...
DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU
link : DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU

soma pia


DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU

Na Mathias Canal, Geita

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kuwafukuza kazi maafisa watatu wa idara ya Maendeleo ya Mazao katika sehemu ya pembejeo ambao wamebainika kuhusika moja kwa moja na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita Mhe Tizeba alisema kuwa kufukuzwa kazi kunajili kutokana na ukosefu wa umakini na usimamizi mzuri wa sheria ya ununuzi wa Umma ikiwemo kusababisha kuchapishwa kwa vocha za pembejeo zenye thamani ya Tshs 78,054,970,000 ambazo ni zaidi ya bajeti halisi iliyotengwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa kiasi cha Tshs 42,587,419,200

Watumishi waliofukuzwa kazi ni Bw Shenal S. Nyoni aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha pembejeo, Aliyekuwa Afisa kilimo Daraja la I Bw Michael G. Mayabu na Bw Franks F. Kamhabwa.

Waziri Tizeba ametumia mamlaka hayo mara baada ya kupitia taarifa ya waraka wa mkakati wa utekelezaji na Usimamizi wa utoaji wa Ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa kutumia vocha wa mwaka 2015/2016 ambapo pamoja na mambo mengine uliainisha utaratibu wa usimamizi wa zoezi la utopaji wa ruzuku ambao ulilenga kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.



Hivyo makala DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU

yaani makala yote DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dkt-tizeba-afukuza-kazi-watatu-atoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU"

Post a Comment

Loading...