Loading...
title : DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
link : DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Na Mathias Canal, Geita
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo Octoba 16, 2017 amefunga rasmi maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16, mwaka 2017.
Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho hayo waziri Tizeba alisema kuwa Kuanzia msimu huu wa kilimo Wakulima wa korosho watapata bure pembejeo aina ya salfa zilizokuwa zikiuzwa kwa bei ya ruzuku.
Alisema Hatua hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa, vikiwakabili Wakulima wa zao la korosho vinaondolewa ili kuwawezesha kuongeza uzalisha na tija zaidi kutokana na zao hilo.
Mhe Tizeba alisema Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ni kutoa nafasi ya kutafakari, namna Jamii katika ngazi ya Kaya, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, Taifa na Kimataifa zinavyoweza kuhakikisha ongezeko la uzalishaji na upatikanaji wa chakula cha kutosha na chenye lishe bora kwa watu wote na kwa wakati wote.
Alisema kuwa Kila mwaka Shirika la Chakula Duniani (FAO) baada ya kufanya tathmini ya hali ya Chakula hutoa Kaulimbiu ambayo huwa ni dira ya maandalizi na maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alipotembelea banda la Kampuni ya POLYTECH MACHINERY inayojishughulisha na uuzaji wa mashine mbalimbali ikiwemo za kukamua mafuta ya alizeti wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita. Mwingine ni Mhe Dkt Mary Mwanjelwa Naibu waziri wa Kilimo (Kulia).
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Hivyo makala DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
yaani makala yote DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/dkt-tizeba-afunga-maadhimisho-ya-siku.html
0 Response to "DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI"
Post a Comment