Loading...
title : MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017
link : MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017
Mkoa wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi Oktoba.
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike yamehudhuriwa na watoto kutoka maeneo na shule mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa serikali na vyama vya siasa,wananchi na mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali likiwemo shirika la kimataifa la Save the Children.
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya “Tokomeza Mimba za utotoni,Tufikie uchumi wa viwanda”.
Akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini hivyo jitihada mbalimbali zinahitajika kuhakikisha mimba za utotoni zinatokomezwa mkoani humo.
Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akitoa hotuba katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini leo Oktoba 11,2017.Picha zote Kadama Malunde- Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima aliwataka wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ya Chagulaga ambayo wanaume hutumia fursa kuchagua mchumba na kusababisha watoto wa kike waolewa bila ridhaa yao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Ngassa Mboje akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Iselamagazi wakiimba na kucheza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017
yaani makala yote MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/maadhimisho-ya-siku-ya-kimataifa-ya_11.html
0 Response to "MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017"
Post a Comment