Loading...
title : MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA.
link : MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA.
MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA.
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto UMMY MWALIMU (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam, pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt FAUSTINE NDUGULILE (kulia).
Waziri wa Afya UMMY pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt FAUSTINE wakipokea vifaa ivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali vitakavyotoa huduma hizo
Mwambawahabari
Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.
Akiongea na waandishi wa habari leo Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto UMMY MWALIMU amesema vituo vya afya vihakikishe vinatenga siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.

"Wanawake wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia kupunguza saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi kwa kina mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa kubwa ". Amesema
Amesema katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.
Aidha Waziri ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba na kuwataka kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani ila zinatuliza tu.
" Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache tabia ya kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni kweli inatibu". Amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt FAUSTINE NDUGULILE amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.
"Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020".Amesema.
Hivyo makala MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA.
yaani makala yote MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/matibabu-ya-saratani-ya-matiti-kutolewa.html
0 Response to "MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KUTOLEWA BURE NCHINZIMA."
Post a Comment