Loading...

MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR

Loading...
MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR
link : MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR

soma pia


MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR




NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
TIMU ya soka ya wafanyakazi wa Mwalimu Commercial Bank,(MCB), plc, imefungwa mabao 3-1 na kikosi mchanganyiko cha walimu wa jijini dar es salaam, katika pambano la kirafiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya wiki moja ya walimu wa michezo yaliyofanyika chuo kikuu cha dar es salaam.
Pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, leo Oktoba 21, 2017, haikuwa kazi rahisi kwa kombaini ya walimu kushinda mchezo huo dhidi ya “mabenker” hao wa MCB, kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote zilitoka sare ya bao 1-1.
Katika kipindi cha pili tena dakika za lala salama, wafanyakazi wa MCB walielemewa na kujikuta wanatundikwa mabao mawili ya haraka haraka.
Hata hivyo kocha wa MCB, Lufingo Mwakilasa, aliwasifu wachezaji wake kuwa wamejitahidi kucheza vizuri licha ya hali ya hewa kuwa mbaya (joto kali), lakini pia asili ya kazi yao ambayo muda mwingi huwa wanautumia wakiwa maofisini kuhudumia wateja ukilinganisha na wenzao ambao ni walimu wa michezo na muda mwingi huwa wanafanya mazoezi.
Akizungumzia pambano hilo la kirafiki, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Valence Luteganya alisema, kwa takriban wiki moja walimu hao wa michezo walikuwa wakishiriki semina ya mafunzo chuo kikuu ambayo MCB ilidhamini semina hiyo.
“Mchezo huu ni wakujenga ushirikiano wa karibu na wenzetu walimu, ambao nao ni wateja wetu wakubwa.”alisema Lutenganya.

Kombania ya walimu wa michezo wa jiji la Dar es Salaam, ambao walimenyana na wafanyakazi wa MCB katika pambano la soka la kirafiki.

Mchezaji wa MCB, (Kulia), akimenyana na mwenzake wa kombania ya Walimu.

Priva Audax wa MCB, akijikunjua kufumua shuti.




Kocha mkuu wa MCB, Lufingo Mwakilasa

Wachezajiwa MCB (kulia), wakisalimiana na wwenzao wa Kombania ya walimu wa Dar es Salaam tayari kuanza mchezo huo.

Kipa wa MCB, akiruka kuokoa mpira

Kipa wa MCB, akipangua mpira

Priva Audax wa MCB


Hivyo makala MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR

yaani makala yote MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/mcb-yashiriki-bonanza-la-michezo-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR"

Post a Comment

Loading...