Loading...
title : SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA
link : SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA
SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA
Serikali imewatoa hofu wafugaji nchini kuhusu mchakato wa upigaji chapa wa mifugo na kusema kuwa mpango huo haulengi kuchukua mifugo bali Serikali inataka kubaini mifugo iliyopo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa hofu jana wakati akizungumza na wakulima na wafugaji wa kijiji cha Perani wilayani Mkinga mkoa wa Tanga.
Kauli hiyo ya Ulega imekuja baada wafugaji wa Perani kumweleza kwamba hawana elimu ya kutosha kuhusu mchakato huo na kwamba wanahisi kama mifugo yao inachukuliwa na Serikali .
Ulega amesema Serikali ya Awamu ya Tano, ni sikivu na imedhamilia kuwatumikia vyema Watanzania na siyo kuwanyonya wananchi wa Taifa.
"Rais wetu ni mtu wa wanyonge, hakuna mtu yoyote atakayechukuliwa ngo'mbe zake.Bali tunataka kujua mifugo yote iliyopo ili kuzuia mwingiliano na ile inayotoka nchi za jirani,"amesema Ulega.
Naibu waziri huyo, ametumia nafasi hiyo kuwasihi wafugaji na wakulima wa eneo hilo kuacha mapigano baina yao kwani siyo jambo zuli na halileti taswira nzuri
"Naomba muishi kwa amani na utulivu kuanzia leo tatizo lenu nitalifikisha ngazi ya juu kuanzia kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela ili atume wataalamu waje kuangalia namna ya kusimamamia vyema mpango kazi,"amesema Ulega.
Awali mwenyekiti wa kijiji hicho, Letinga Oyaya alimweleza naibu waziri huyo kwamba wanaomba kuelimishwa namna ambayo mchakato wa upigaji chapa utakavyotekelezwa na madhumuni yake.
Hivyo makala SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA
yaani makala yote SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/serikali-haina-nia-ya-kuchukua-mifugo.html
0 Response to "SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA"
Post a Comment