Loading...

SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

Loading...
SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA) - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)
link : SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

soma pia


SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

Benny Mwaipaja, Kagera.

NAIBU waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameziagiza Mamlaka na Taasisi zote za Umma kufanya ununuzi wa vifaa na mafuta kupitia Wakala wa Serikali wa ununuzi na ugavi (GPSA) kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na kuwaonya wahusika wote watakaoendelea kukaidi maagizo hayo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo mkoani Kagera baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoani humo na kubaini kuwa taasii na idara nyingi za umma zinafanya manunuzi nje ya mfumo wa GPSA jambo ambalo amesema ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.

Alisema kuwa lengo la Serikali la kuanzishwa kwa wakala huo pamoja na mambo mengine ilikuwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali haitakubali kuona sheria zinakiukwa kwa makusudi na kwa malengo yanayoonesha kuna nia isiyo njema katika matumizi ya fedha za umma.

“Hili si ombi ni maelekezo na ni agizo, taasisi zote zipate huduma kutoka kwa wakala wetu (GPSA) kwani Serikali ilikuwa na dhamira ya uwepo wa matumizi sahihi ya fedha za matumizi wanazopelekewa na ndiyo maana ukaanzishwa Wakala huu” Alisema Dkt. Kijaji
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Kaimu Meneja  wa Wakala Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi, kuhusu kuwahudumia Taasisi zote za Serikali kwa kuwa ndio wajibu wa Wakala huo, alipofanya Ziara katika Ofisi hizo za Mkoani Kagera.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akielezea namna atakavyoshirikiana na Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini katika Mkoa huo ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi adili ya fedha za Serikali, Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi za Wakala huo Mkoani Kagera.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) namna tetemeko la ardhi lilivyo haribu miundombinu ya Ofisi hizo, alipotembelewa na Naibu Waziri huyo katika Ofisi za GPSA Mkoani humo.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba  Bw. Deodatus Kinawiro (kulia) akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) alipotembelea Ghala la Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoani Kagera.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

yaani makala yote SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/serikali-yazionya-taasisi-za-umma.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)"

Post a Comment

Loading...