Loading...
title : Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo
link : Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo
Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limepata mtambo wa uchorongaji kwa kutumia upepo (Air Rotary Drill Rig) wenye thamani dola za Kimarekani milioni 1.3 utakaotumika kupata taarifa za kijiolojia na mashapo kwa wachimbaji wadogo .
Kunufaika kwa wachimbaji wadogo kutatokana na Stamico kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico, Balozi Alexender Muganda amesema kuwa mtambo umetengenezwa nchini Canada na utasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za kjiolojia na mashapo katika maeneo yao kwa gharama nafuu.
Amesema mtambo huo umetolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini chiini ya ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa usimamizi endelevu wa rasilimali ya madini Tanzania (SMMRP). Balozi Muganda amesema mtambo huo una uwezo wa kuchoronga miamba kwa kutumia upepo na kwa haraka zaidi kati ya kina cha mita 30 hadi 200 na kwa gharama ambazo mchimbaji mdogo atamudu na kuachana na uchimbaji wa kubahatisha pamoja kuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha. Aidha amesema kuwa wachimbaji wadogo wanaohitaji huduma za uchorongaji kwa kutumia upepo wafike katika ofisi za Stamico ili kupata taarifa zaidi.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji Bw. Alex Rutagwelela akiangalia mtambo huo wa uchorongaji wa miamba baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico Balozi Alexander Muganda akizungumza na waandishi habari juu shirika la Taifa la Madini (Stamico) kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji kwa kutumia upepo , jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo
yaani makala yote Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/stamico-yaleta-mapinduzi-kwa-wachimbaji.html
0 Response to "Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo"
Post a Comment