Loading...
title : TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI
link : TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI
TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano wa kibiashara na Tanzania alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza jambo aliokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani) alipokua akizungumzia mazingira bora ya kibiashara kwa maendeleo ya Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akieleza kuhusu uimara wa Serikali katika kusimamia mazingira bora ya biashara ili kusaidia kuinua Sekta binafsi nchini, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi (kulia) akizungumzia masuala ya kodi katika Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga.
moja wa wajumbe walioongozana na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza Bw. Lord Clive Hollick (kushoto), mkutano huo umefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia), Mwakilishi wa Biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (wa nne kushoto) na Maafisa waandamizi kutoka Uingereza na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kuhusu Biashara kati ya nchi hizio mbili Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WFM)
Hivyo makala TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI
yaani makala yote TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tanzania-na-uingereza-zajadiliana.html
0 Response to "TANZANIA NA UINGEREZA ZAJADILIANA KUHUSU BIASHARA NA UWEKEZAJI"
Post a Comment