Loading...

Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla

Loading...
Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla
link : Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla

soma pia


Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka viongozi wa Serikali na wale wenye upande wa mgogoro wa pori tengefu la Loliondo kukaa chini ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lililochukua karibu miaka zaidi ya 20 sasa huku akitoa tamko la kusitisha operesheni zote zilizokuwa zikiendelea katika suala hilo.
Waziri Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo kwenye mkutano wa wazi Oktoba 26,2017 wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo wakiwemo wale wenye mgogoro na pori hilo.
“Kuanzia leo, mimi kama Waziri wa Maliasili na Utalii, nina waahidi kufanya uhifadhi endelevu, kukaa na wananchi kuhifadhi. Hivyo nawaomba viongozi wa Serikali na wananchi kwenye mgogoro huu sasa kufikia mwisho na kukaa meza moja.
Mgogoro utatatuliwa kwa kukaa mezani. Kwa pande zote mbili sasa kuja na jibu moja juu ya kusitisha mgogoro huu. Hatutaki tumuone Mkuu wa Wilaya mbaya ama Mkurugenzi wake ama wahifadhi wabaya au Waziri wa Maliasili  bali, sote tuwe kitu kimoja katika meza ya majadiliano na kufikia mwisho” alieleza Dk.Kigwangalla.
Ameongeza kuwa:
“Tutasimamia kushirikiana na nyie. Lakini hatutokubalana na watu miongoni mwetu wa watu ambao wataivunja sheria kwa makusudi. Kwa msingi huo, napenda kutamka kuwa, nasitisha operesheni iliyokuwa ikiendelea Loliondo ile ya kukamata wafugaji na kuwatesa ama vitendo vingine vibaya. 
Pili naagiza watalaam wa maji, wakae na watalaam wa hifadhi washirikiane na serikali ya kijiji wawaruhusu wafugaji kunywesha mifugo yao.
Pia naagiza kwa Wahifadhi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, mifugo yote ambayo imekamatwa na mamlaka ambayo ipo chini ya Wizara ambayo nasimamia mimi ile yote ambayo haijahukumiwa na mamlaka za kisheria iachiwe huru kwa wenyewe  kwa  mifugo ambayo itabaki chini ya idara iliyopo kwenye wizara yangu ni ile yenye migogoro ya usuluhishi tu” alieleza Dkt.Kigwangalla.
Waziri Dkt.Kigwangalla yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)mjini Arusha, na baadae Mamlaa ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa namna ya kitatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani


Hivyo makala Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla

yaani makala yote Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tatizo-la-msingi-la-mgogoro-wa-loliondo_28.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tatizo la msingi la mgogoro wa Loliondo litatatuliwa mezani - Dkt. Kigwangalla"

Post a Comment

Loading...