Loading...
title : Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar
link : Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar
Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar kanda ya Unguja imeanza rasmi jana kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan, lakini wapenzi wa Soka wamekijia juu Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) baada ya kuziuza tiketi kwenye michezo hiyo tiketi ambazo zimeshapita muda wake tangu msimu uliopita.
Mashabiki hao wa soka walishangazwa kununua tiketi ya mechi kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya KMKM na badala yake wakauziwa tiketi zilizoandikwa mchezo wa Jang’ombe boys na Taifa ya Jang’ombe mchezo ambao tayari umeshachezwa tangu tarehe 30/07/2017.
Mbali na hilo tiketi wameuziwa shilingi elfu mbili wakati bei iliyoandikwa kwenye tiketi hizo ni shilingi elfu moja.
Mtandao huu umemtafuta mmoja wa kiongozi wa ZFA na kusema kwamba kwa hilo hana ufumbuzi nalo mpaka wahusika zaidi watowe ufafanuzi.
“Mimi mambo hayo ya tiketi siyajuwi kwa undani, wapo wahusika wakuu ndo wanaweza kulitolea ufafanuzi, lakini kwetu Zanzibar mbona naona jambo la kawaida mno si la kushangaza”. Alisema.
Hivyo makala Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar
yaani makala yote Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tiketi-za-zfa-zazua-gumzo-zanzibar.html
0 Response to "Tiketi za ZFA zazua gumzo Zanzibar"
Post a Comment