Loading...
title : TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA.
link : TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA.
TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA.
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Taboea (TUWASA) imewaagizwa kushirikiana na Manispaa ya Tabora kuhakikisha hakuna mtu anaingia katika chanzo cha maji baada ya kuwaondoa wavamizi wote waliokuwa wamejenga katika eneo la Tuku tuku jirani na Shule ya Wasichana ya Tabora.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora mara baada ya kuongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo kutembelea Bwawa la Igombe ili kujionea hali ya uzalishaji maji.
Alisema kuwa eneo hilo linaweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Tabora ambapo hivi sasa wanapata maji kwa njia ya mgao baada ya maji katika Bwawa la Kazima na Igombe kupungua.
Mwanri alisema kuwa baada ya zoezi lilifanyika juzi la kuwaondoa wavamizi wa eneo la Shule ya Wasichana ya Tabora kukamilika , kinachofuata ni kuhakikisha kuwa sehemu ya eneo hilo ambalo ni chanzo maji na lina visima 12 linazungushiwa wigo ili kuzia wavamizi wanaingia ndani yake na kuendesha shughuli zinazosababisha uharibifu.
Alisema kuwa katika hali ilivyo hivi sasa ambapo wakazi wa Manispaa ya Tabora wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji kama eneo hilo lingekuwa halijavamiwa basi lingesaidia kupunguza adha kwa wananchi katika kipindi hiki cha upungufu wa maji katika Bwawa la Igombe na Kazima.
Mwanri alisema kuwa kipindi hiki cha tatizo la maji , visima hivyo vinaweza vikatumika kuwapunguzia wananchi mgao kama wataviwekea utaratibu mzuri ikiwemo kuvilinda visivamiwe.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA Mhandisi Mkama Bwire alisema kuwa wataendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali kuwaondoa watu wote ambao wanaendesha shughuli katika vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaendelea kupatikana kwa wakazi kwa Manispaa ya Tabora.
Alisema kuwa wavamizi hao wamekuwa wakati mwingine wamekuwa wakivizia kipindi ambacho watendaji wa TUWASA hawapo wanaingiza mifugo katika Bwawa la Igombe kwa lengo la kunywesha ng’ombe zao.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA ametoa wito kwa Wakazi wa Manispaa ya Tabora wanaotumika maji yanayozalishwa na Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa wanachemsha maji kabla ya kunywa ili kuchukua tahadhari.
Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kuwa maji hayo yanapita sehemu mbalimbali kabla ya kuwafikia wateja wao na wakati mwingine yanaweza kupita sehemu isiyo salama
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliongoza Kamati yake kutembelea ili kujionea hali ya uzalishaji wa maji na ubora na usalama wake katika matumizi ya wakazi wa Manispaa katika kipindi hiki cha uhaba wa maji.
Alisema kuwa ni vema tahadhari zikachukuliwa kuwaelimishwa juu ya kuyachemsha kabla ya kunywa ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa.
Hivi sasa TUWASA inatumia gharama kubwa sana katika kuhakikisha maji walau yakuwa safi kwa sababu ya Bwawa la Igombe kupungua maji na kubaki tope .
Hivyo makala TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA.
yaani makala yote TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tuwasa-yaagizwa-kujenga-uzio-kuzunguka.html
0 Response to "TUWASA YAAGIZWA KUJENGA UZIO KUZUNGUKA CHANZO CHA MAJI CHA SHULE YA WASICHANA TABORA."
Post a Comment