Loading...

UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA

Loading...
UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA
link : UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA

soma pia


UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezungumzia umuhimu kwa wafanyakazi wote waliopata fursa ya kujenga reli ya kisasa (SGR) kufanya kazi kwa moyo na uzalendo mkubwa ili kuandika historia katika maendeleo ya Tanzania.
Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka viongozi wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye  Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi  kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.
Takribani shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa usafiri wa reli hapa nchini.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah Kilic, anayejenge reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani. 
 Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mhandisi Maizo Mgedzi, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani, inayojengwa usiku na mchana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akimpongeza mwanamke anayeendesha mtambo wa kutengeneza tuta la reli ya kisasa (SGR), Bi Miriam Juma alipomkuta saa 4 za usiku akichapa kazi katika eneo la Soga, mkoani Pwani.
Muonekano wa Mitambo ya kisasa inayojenga Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga mkoani Pwani, inayojengwa kwa saa 24. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Hivyo makala UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA

yaani makala yote UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/ukaguzi-reli-ya-kisasa-usiku-waleta.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA"

Post a Comment

Loading...