Loading...

VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE

Loading...
VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE
link : VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE

soma pia


VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE

Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa utendaji kazi na kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe.

Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali hapa Dodoma Mjini na kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Michezo na Uwezeshaji wananchi.

Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.

Kwa upande wake, Mavunde akizungumza katika Dua hiyo, amewashukuru Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.

Mavunde ameipa Misikiti 16 Spika moja kila mmoja zenye thamani ya Tsh 4,000,000 na pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa kwenye picha na viongozi wa dini.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisikiliza mawaidha katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.


Hivyo makala VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE

yaani makala yote VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/viongozi-wa-dini-ya-kiislamu-wampongeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE"

Post a Comment

Loading...