Loading...

WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

Loading...
WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA
link : WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

soma pia


WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

Benny Mwaipaja, Karagwe
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewataka wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar) kuchangamkia soko la uhakika la zao hilo kwa  kuongeza uzalishaji wa miwa kutokana na uhitaji mkubwa wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa miwa katika kiwanda hicho

Dkt. Kijaji alitoa wito huo baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuelezwa kuwa katika msimu wa kilimo cha miwa uliopita wakulima wa miwa wanaozunguka kiwanda hicho walilipwa Shilingi bilioni 4 baada ya kukiuzia kiwanda hicho zaidi ya tani 56,000 za miwa.

Alisema kuwa bado mahitaji ya miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari kiwandani hapo ni makubwa na kuwataka wakulima hao kupitia umoja wao wa wakulima wadogo wa miwa kuhamasishana kuongeza uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kiwanda cha Sukari cha Kagera kimeendelea kuongeza uzalishaji tangu kipate wawekezaji ambapo uzalishaji huo umeongezeka kutoka tani 25,000 mwaka 2011/2012 hadi kufikia tani 75,000 na katika kipindi cha miaka mitano ijayo uzalishaji utafikia tani 170,000.

Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kiwanda hicho Bw. Ashwin Rana alisema wameanzisha Kitengo maalumu cha kuwaendeleza wakulima wadogo wa miwa wanaozunguka mashamba yao kwa kuendelea kuwapatia vitendeakazi ikiwemo matrekta, utaalamu pamoja na mbegu bora za miwa ili waweze kuchangia kuzalisha miwa yatakayosaidia waweze kufikia malengo yao ya kuongeza uzalishaji wa sukari.

Bw. Rana alisema kuwa tangu walipoanza kuunda umoja wa wakulima wadogo wa miwa wanaozunguka mashamba yao mwaka 2006, uzalishaji wao umeongezeka kutoka tani 0 hadi tani 56,000 ambazo kiwanda hicho kilinunua msimu uliopita na kwamba wanatarajia uzalishaji wao utaongezeka zaidi.

“Mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 450,000 lakini uzalishaji uliopo hivi sasa ni tani 320,000 na kwa mikakati ya Kiwanda cha Sukari Kagera ya kuongeza mashamba na teknolojia ya uzalishaji wa bidhaa hiyo utapunguza kwa kiasi kikubwa upungufu huo” aliongeza Bw. Rana.

Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Beatus Nchota, alieleza kuwa Mamlaka hiyo inapongeza jitihada kubwa ya kiwanda hicho kuongeza uzalishaji hatua ambayo itaongeza mauzo, ajira na hatimaye kuongeza kiwango cha kodi ambayo Kiwanda hicho kimekuwa kikilipa kwa kiwango kikubwa.


Hivyo makala WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

yaani makala yote WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/wakulima-wa-miwa-kagera-waaswa_19.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA"

Post a Comment

Loading...