Loading...

Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018

Loading...
Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018
link : Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018

soma pia


Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018


Alhamisi, Oktoba 26, 2017

Waombaji wa Mwaka wa Kwanza

Kiasi cha shilingi bilioni 72.2 mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 21,677 kati ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 108.8 kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 8,323watapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 36.6 katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.

Idadi ya wanafunzi 21,677 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika; ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 30,000wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz  na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.

Wakati huo huo, Bodi imeendelea kutoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo na ambao wamefaulu masomo yao ya mwaka wa masomo 2016/2017.

Jumla wanafunzi 54,936 wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu wamepatiwa mikopo mpaka sasa na taarifa zao kuwasilishwa kwenye vyuo husika.

Bodi inatarajia kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 123,295 kwa mwaka wa masomo 2017/2018 wakiwemo wa mwaka wa kwanza 30,000 na wanaoendelea na masomo wapatao93,295.

  
Hitimisho
Bodi ya Mikopo inawasisitizia waombaji wa mikopo kuendelea kuwa na subira wakati ikikamilisha orodha inayofuata ya wanafunzi waliopata mikopo na itaendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na tovuti ya Bodi mara kwa mara.
Mwisho.
Imetolewa na:
ABDUL-RAZAQ BADRU
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
ALHAMISI, OKTOBA 26, 2017


Hivyo makala Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018

yaani makala yote Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/wanafunzi-11481-wapata-mikopo-awamu-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wanafunzi 11,481 Wapata Mikopo Awamu ya Pili .2017-2018"

Post a Comment

Loading...