Loading...
title : WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF
link : WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF
WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF
Makocha 28 wanawake kutoka vyuo mbalimbali vya Maendeleo ya Jamii nchini leo Oktoba 17, 2017 wamehitimu kozi fupi ya ukocha katika kozi iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO).
Kozi hiyo ya siku mbili ambayo ni ya pili kufanyika kwa makocha hao, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume - Makao Makuu ya TFF ilikuwa chini ya mkufunzi wa TFF, Raymond Gweba.
Akizungumza kwenye ufungaji wa kozi hiyo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali inafahamu kuwa inatakiwa kuwekeza kwenye soka la wanawake kuanzia upande wa vijana na ndio maana inatengeneza mazingira na sera zitakazowezesha mafanikio hayo.
Singo amesema nchi mbalimbali wana maendeleo makubwa katika mpira wa miguu kwa wanawake na sasa wakati wa Tanzania kuwekeza katika upande huo kuanzia kwa watoto na makocha.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akiwa anamsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi wakati wa ufungaji wa kozi ya wanawake iliyoendeshwa kwa muda wa siku 2, kulia ni Ulf Kjellstig na Mwenyekiti wa soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo akikabidhi cheti na vifaa vya michezo kwa moja ya washiriki wa kozi ya ukocha kwa wanawake leo Jijini Dar es Salaam, sambamba na Mwenyekiti wa Soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma Ulf Kjellistig.
Hivyo makala WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF
yaani makala yote WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/wanawake-28-wahitimu-kozi-ya-ukocha-tff.html
0 Response to "WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF"
Post a Comment