Loading...

Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika

Loading...
Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika
link : Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika

soma pia


Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika

Waogeleaji wa Tanzania, Sonia Tumitto, Collins Saliboko, Hilal Hilal na Emma Imhoff (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na waogeleaji kutoka Zambia na Kenya mara baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwa upande wa Relay.

Waogeleaji wa Tanzania wameendelea kung’ara katika mashindano ya Cana ya Kanda ya tatu ya Afrika baada ya kuendelea kukusanya medali mbalimbali kwa siku ya pili mfululizo. Kutokana na kutawala mashindano hayo, matumaini ya timu hiyo ya Taifa kulitetea kombe hilo yameongezeka na wanatarajia kuweka historia ya pili kwa kutwaa ubingwa wa jumla wa mashindano hayo.

Siku ya kwanza, Tanzania ilitwaa medali zaidi ya 21, huku ikishinda medal tisa za dhahabu, tano za shaba na saba za fedha katika mashindano hayo yanayoshirikisha jumla ya nchi sita ambazo ni Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Sudan na wenyeji Tanzania.

Muogeleaji wa kwanza wa Tanzania kutwaa medali ya  dhahabu ni Natalie Sanford ambaye alishinda mita 800 kwa staili ya freestyle kwa waogeaji waliochini ya miaka 14 na baadaye muogeleaji nyota wa Tanzania wa kike, Sonia Tumiotto akishinda kwa waogeleaji wa kike wenye umri zaidi ya miaka 15.

 Waogeleaji wengine waliotamba na kutwaa medali za dhahabu ni, Elia Imhoff, Natalie, Emma Imhoff, Tara Behnsen, Marin De Villard na kwenye ‘relay’ kupitia kwa Sonia Tumitto, Collins Saliboko, Hilal Hilal na Emma Imhoff.
Kocha wa timu hiyo, Michael Livingstone alisema kuwa wana matumaini makubwa ya kutetea ubingwa huo pamoja na upinzani mkali kutoka kwa nchi shiriki hasa Zambia.

“Mashindano ni magumu sana, ushindani ni mkubwa, tuna uhakika asilimia 100 kuwa tutashinda, waogeleaji wetu wamefanya vyema katika mashindano ya awali na tunaongoza kwa kutwaa medali,” alisema Michael. Alisema kuwa wamefuraishwa sana na jinsi waogeleaji wao wanavyojituma kwa kutambua kuwa wapo nyumbani nna kukataa kata kata kushindwa.

Mashindano hayo yaliyoanza Alhamis, yatafungwa kesho Jumamosi saa 11.00 jioni na ambapo zawadi mbalimbali za washindi zitatolewa.
Waogeleaji wakijiandaa ‘kuchumpa’ katika mashindano ya kuogelea ya Cana Kanda ya Tatu Afrika.
Muogeleaji wa Kike wa Tanzania Kayla Temba akipigania medali katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu.


Hivyo makala Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika

yaani makala yote Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/watanzania-waendelea-kuzoa-medali.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Watanzania waendelea kuzoa medali kwenye mashindano ya kuogelea Cana kanda ya tatu Afrika"

Post a Comment

Loading...