Loading...

Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.

Loading...
Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.
link : Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.

soma pia


Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.

Wanachama wa Chama cha Wawekezaji Binafsi kwenye Elimu TAPIE , wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, alipokuwa akifungua mkutano wao  Mkuu Maalum mkoani Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
WAZIRI Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, amesifu mchango wa shule binafsi kwa juhudi kubwa wanazofanya  katika kuiinua sekta ya elimu hapa nchini.

Jaffo alitoa sifa hizo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa siku moja wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIE), uliofanyika Jijini Mwanza.

Alisema mchango wa shule hizo umesaidia  kuifanya Tanzania ionekane kuwa iko katika hali nzuri kielimu kwa kutoa vijana waliofuzu kimasomo na kuwa na uwezo  kuiwakilisha katika mikutano mbalimbali ya nchi za nje.

Mkutano huo wa siku moja ulikuwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha sekta ya elimu kwa kuwaleta pamoja wawekezaji na wamiliki wa shule binafsi kuwa na jukwaa la mijadala na midahalo kuhusu uendeshaji wa shule na maslahi ya jamii nzima.

 “Kiukweli Shule binafsi zimekuwa zikisaidia kwa  kiwango kikubwa katika kuinua elimu ya nchi yetu kwa kutoa vijana waliofuzu vizuri kimasomo na kuipatia sifa Tanzania, ingwa mnafanya vizuri niwaombe muwe waminifu katika kipindi hiki cha mitihani ya kidato cha nne inayotarajia kuanza hivi karibuni, ,”Jaffo.

Naye Rais wa (TAPIE) Ester Mahawe ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), alisema Serikali na wananchi kwa ujumla watambue  taasisi hiyo ni chombo kinachowapatia fursaa wamiliki kuwa sehemu ya uandaaji wa sera, miongozo na sheria, za kuendeshea, kuwa kiungo muhimu na mshiriki wa kuisaidia serikali  katika kuongeza fursa ya elimu kwa vijana wa Kitanzania na uboleshaji wa utoaji wa elimu hapa nchini.

“TAPIE  inahakikisha maslahi ya wamiliki wa shule binafsi hapa nchi yanalindwa na kutetewa katika ngazi na idara zote za serikali na ikumbukwe changamoto za uwekezaji katika sekta ya elimu ni nyingi sana,kuanzia umiliki wa ardhi,kodi na tozo mbalimbali,” alisema na kuongeza

“Sheriia na miongozo isiyo rafiki kwa wamiliki, gharma za wafanyakazi, mikopo yenye riba kubwa nk, hivyo kwa sasa tunahitaji chombo chenye maono na dhamira ya dhati ili kuona mitaji yetu na nguvu zetu zinazotumika zinakuwa na tija na zinalindwa kimfumo,”alisema Mahewa.


Hivyo makala Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.

yaani makala yote Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/waziri-jaffo-afagilia-mchango-wa-shule.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi."

Post a Comment

Loading...