Loading...

Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma

Loading...
Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma
link : Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma

soma pia


Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma


Eliphace Marwa-MAELEZO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezindua bodi mpya ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma mapema jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo waziri Kairuki ameitaka bodi hiyo kuzingatia misingi iliyopo kwenye hati maalum ya Rais ambayo inawataka kuzingatia vigezo ambavyo ni pamoja na malipo ya mishahara na masilahi kwa watumishi wa Umma yanapatikana na kuwa endelevu.

“Ni vema kuhakikisha utumishi wa Umma unavutia na kubakiza taaluma zinazohitajika katika kuendesha shughuli zake ili kuweza kuleta tija kwa kuzingatia uwazi, usawa na haki mahala pa kazi”, alisema Waziri Kairuki.Aliongeza kuwa endapo bodi itazingatia vigezo hivyo, ushauri watakaoutoa utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na hivyo kujenga imani kwa watumishi wa Umma na wadau wengine.

Waziri Kairuki aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa bodi hiyo na kusema kuwa Serikali iko pamoja nayo katika kuhakikisha masiilahi ya watumishi wa Umma yanaboreshwa ili kuongeza tija kwa kuwabakiza wataalam katika Utumishi wa Umma.Naye Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza kwa kwa kufanya tafiti.

“Napenda kusema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika bodi tutashirikiana na Serikali katika kuboresha hali ya utendaji katika utumishi wa Umma kwa kufanya tafiti kwa lengo la kuishauri Serikali ili iweze kuwapatia maisha ya staha Watumishi wa Umma”, alisema Ndagula.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma pamoja na Sekretarieti ya bodi hiyo wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma

yaani makala yote Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/waziri-kairuki-azindua-bodi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma"

Post a Comment

Loading...