Loading...
title : WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI
link : WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI
WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.
Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.
“Mimi nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.
Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
“Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI
yaani makala yote WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/waziri-mbarawa-awataka-wafanyakazi.html
0 Response to "WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI"
Post a Comment