Loading...
title : Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif
link : Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif
Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif
Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq wa kwanza kutoka Kushoto aliyefika Zanzibar kujitambulisha rasmi wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekaa kati kati Ofisi Vuga Mjini Zanzibar.
Wa kwanza kutoka Kulia ni Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dr. Ahmed Hamood Al – Habsi akifuatiwa na Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akimzawadia Mlango Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq kama ishara ya kufungulia Milango ya uwepo wake Nchini Tanzania.
Balozi Seif wa Pili Kutoka Kulia akiwa katika Picha ya pamoja na Mabalozi wa Oman wanaofanya kazi Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Visiwa vya Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq na Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga.
Kushoto ya Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dr. Ahmed Hamood Al – Habsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Picha na – OMPR –ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar na Oman zitaendelea kufanya kazi pamoja katika dhana nzima ya kudumisha ushirikiano wa Damu uliopo wa muda mrefu kwa maslahi ya maendeleo ya Kiuchumi na ustawi wa jamii wa Wananchi wa Mataifa hayo mawili.
Alisema Ushirikiano huo umeimarika zaidi kwa Zanzibar kupokea ufadhili wa Vijana wake wanaopata fursa za kujiunga na Masomo ya juu Nchini Oman katika fani mbali mbali za mafunzo ikiwemo Udaktari, Uhandisi, Kompyuta pamoja na Lugha.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq aliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi akiambatana pia na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dr. Ahmed Hamood Al - Habsi.
Alisema Zanzibar inafurahia kuendelea kuwepo kwa uhusiano huo wa kipekee na wa kupigiwa mfano ambao umekuwa ukileta faraja na matunda mazuri yanayotowa fursa zaidi kwa Zanzibar kutanua wigo wa Kimaendeleo na kuongeza maeneo mengine ya ushirikiano wa Kisiasa, Kiuchumi na Kiutamaduni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi Ali Abdulla – Al Mahrouq kwamba uungaji mkono wa Oman kwa Zanzibar hasa katika utanuzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni umeleta faraja kwa Wananchi walio wengi kwenye huduma za Afya zinazotarajiwa kuenea katika masafa yasiyozidi Kilomita Tano.
Balozi Seif aliipongeza Serikali ya Oman kwa msaada wake mkubwa inayoendelea kutoa kwa Zanzibar hasa kwa kukubali kugharamia matengenezo makubwa ya Majengo ya Kihistoria ya Beit el ajab na Jumba la Makumbusho ya Kifalme yaliyopo Forodhani Mjini Zanzibar.
Alisema msaada huo wa Majengo hayo muhimu umekuja wakati muwafaka kwa vile utasaidia kuhifadhi Historia ya Kiutamaduni na Kiutawala ya Visiwa vya Zanzibar inayohusisha pia mafungamano ya Majengo hayo na Oman.
Akigusia ujio wa Meli ya Kifalme ya Fulk Al Salamah kutoka Nchini Oman Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alieleza wazi kwamba Zanzibar imepata faraja kubwa ya ziara ya Ujumbe wa Serikali ya Oman uliowasili Zanzibar na Meli hiyo ya Kifahari.
Alisema Wananchi wa Zanzibar wamepata kujifunza mambo mbali mbali kufuatia ujio wa Meli hiyo kwa kupata taaluma ya kuepuka masuala mazima yanayotokana na Sekta ya mafuta ambayo kwa sasa Visiwa vya Zanzibar vimo katika matayarisho ya awali ya kuendesha Miradi inayotokana na Sekta hiyo.
Akigusia suala la Majanga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameishukuru Serikali ya Oman kwa msaada wake wa kuwawezesha Viongozi Wanne Waandamizi wa Zanzibar kupata fursa ya kujifunza mbinu na Taaluma ya jinsi ya kujikinga na Majanga.
Balozi Seif alisema mafunzo hayo yameleta faida kubwa kiasi kwamba Oman ingefikiria tena kutoa nafasi nyengine kama hizo kwa watendaji wengine wa Taasisi za Majanga Zanzibar kupata fursa kama hizo katika kipindi chengine kijacho.
Mapema Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania Bwana Ali Abdulla – Al Mahrouq alisema udugu uliopo wa Viongozi pamoja na hata Wananchi wa kawaida wa Oman na Zanzibar ni vyema ukaongezeka zaidi katika uhusiano wa masuala ya Kibiashara.
Balozi Al – Mahrouq alisema pande hizo mbili zimekuwa na historia ndefu ya Kiutamaduni na Kisiasa kiasi kwamba kwa sasa nguvu zikaongezwa katika uimarishaji zaidi wa Kibiashara jambo ambalo linaweza kustawisha kuongeza ukaribu wa Wananchi wa pande hizo mbili unaoweza kudumu milele.
Balozi huyo wa Oman Nchini Tanzania alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Serikali ya Oman itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha harakati za Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Wananchi wa Zanzibar unazidi kukua.
Hivyo makala Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif
yaani makala yote Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/balozi-mpya-wa-oman-nchini-tanzania.html
0 Response to "Balozi Mpya wa Oman Nchini Tanzania akutana na Makamu wa Pili wa Rais , Balozi Seif"
Post a Comment