Loading...

BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto

Loading...
BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto
link : BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto

soma pia


BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto


BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.


Akizindua mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.


Alisema mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.


“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” alisema.

Alitoa wito pia kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine kuhakikisha yanaiga mfano huo wa BancABC kwani wizara yake iko tayarikushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akikabidhi moja ya kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu


Hivyo makala BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto

yaani makala yote BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/bancabc-yashirikiana-na-kitengo-cha_26.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto"

Post a Comment

Loading...