Loading...
title : Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji.
link : Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji.
Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania hivi karibuni ilipiga hodi mjini Hong Kong kujadiliana na Taasisi mbali mbali za Hong Kong na China kuhusiana na fursa za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mitaji na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana Francis Assenga walikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makampuni na taasisi kadhaa zikiwamo Benki ya China; China Capital Fund Management (Hong Kong); First Shanghai Capital Ltd; Mwakilishi wa China Africa Industrial Forum Ndugu Wenbao Tan ambaye ni Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha China.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bwana Takashi Kawasaki na Mkurugenzi wa China Biodiversity Conservation and Green Development Foundation Prof. Frederick Charles Dubee.
Miongoni mwa yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na fursa zilizopo kwenye Mikakati ya 'Silk Road Economic Belt and the 21st-century Maritime Silk Road', ujulikanao kama 'One Belt and One Road Initiative' (OBOR) ambapo kwa mujibu wa Mkakati huo, Tanzania ndio lango kuu la kuingilia Afrika kwa fursa hizo za kiuchumi na kibiashara toka Asia ambapo Tanzania inakuwa kama kiungo muhimu hivyo kuweza kunufaika zaidi ya nchi nyingine.
Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kukuza uwekezaji kwenye miundombinu ya aina zote, viwanda vikubwa na vya kati, biashara kati ya Afrika na Asia, na Huduma mbalimbali.
Aidha, Bwana Assenga alikutana pia na akina mama wa shirika lisilo la kiserikali la kukuza uchumi kwa akina mama wa Hong Kong wanamiliki pia Shule ya Sekondari kama mchango wao kwenye huduma za jamii.
Hivyo makala Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji.
yaani makala yote Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/benki-ya-kilimo-yatinga-hong-kong.html
0 Response to "Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji."
Post a Comment